This archive report was first published on 8 August 2019.
Maafisa wa polisi mjini Eldoret wamemtia mbaroni mwanariadha anayecheza Marekani kufatia kifo cha mwalimu wa shule ya upili katika mtaa wa Outspan.
Alama ya kifo ya Gloria Sangutei ilipatikana Jumatatu, Agosti 5, karibu na shamba la mahindi, na mwili huo ulikuwa na alama za kifo.
Polisi walisema mshukiwa, anayedaiwa kuwa mume wa marehemu, alikamatwa na kuzuiliwa baada ya kujisalimisha polisi Jumanne, Agosti 6.
Francis Warui, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Kapseret, alisema mshukiwa alijitokeza katika Kituo cha Polisi cha Kiambaa akitaka kufahamu ikiwa ni mke wake aliyekuwa amepatikana ameuawa katika shamba la Ancilla, Outspan.
Warui alisema, "Mshukiwa alijitokeza katika Kituo cha Polisi cha Kiambaa akitaka kufahamu ikiwa ni mke wake aliyekuwa amepatikana ameuawa katika shamba la Ancilla, Outspan. Lakini alitoa taarifa kinzani alipohojiwa na polisi Langas,".
Warui aliongeza, "Tutamhoji kuhusiana na tukio hilo. Tukipata hakuna uhusiano unaomtia hatiai, ataachiliwa huru."