This archive report was first published on 7 August 2019.
Ann Kansiime, mchekeshaji mashuhuri kutoka Uganda, amefichua kwamba alichangia mume wake kwa mahari yake, jambo ambalo ni kinyume cha desturi ya Kiafrika.
Alisema kuwa alikuwa ameolewa na Gerard Ojok kwenye ndoa iliyodumu miaka mitano kabla ya kuvunjika mwaka wa 2017.
Alisema penzi linapomuingia msichana, basi linaweza kumzungusha pakubwa, na hivyo kuwafanya waweze kukulipia mahari.
Alisema, "Unajua ukimpenda mtu, utafanya chochote ili aweze kukupata... aweze kukulipia mahari. Aweze kupata mahari hiyo."
Alisema alijipatia jina kupitia vipindi vyake kama vile 'Don't Mess with Kansiime' ambavyo vimekuwa maarufu.