KWS Makachero Wakamata Watu Waliokuwa Wakisafirisha 200kgs za Nyama ya Nyati kuelekea Nairobi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 6 August 2019.

KWS Makachero Wakamata Watu Waliokuwa Wakisafirisha 200kgs za Nyama ya Nyati kuelekea Nairobi

Maafisa wa Huduma ya Wanyama Pori (KWS) wamefanikiwa kuwakamata watu watatu waliokuwa wakisafirisha 200kgs za nyama ya nyati kuelekea Nairobi. Tukio hilo lilichukua eneo la shamba la Marula kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Maafisa hao walikamata gari lililokuwa litumike kusafirisha nyama hiyo. Kulingana na ripoti, makachero walifika wakati watu hao wakipakia nyama ya kifaru katika gari ambalo sasa lipo mikononi mwa polisi.

Naibu mkurugenzi wa KWS anayesimamia eneo la Kati mwa Bonde la Ufa Aggrey Maumo alisema, uchunguzi wetu umetufanya kuamini nyama nyingi ya wanyama pori inayoliwa soko la Burma inatokea Naivasha na Gilgil.

Maumo alisema, kuna wanyama wengi nje ya hifadhi na hivyo wafanyabiashara laghai wanatumia fursa hii kuwaua na kuwauzia wateja wasiokuwa na ufahamu.

Maumo aliendelea kusema kuwa, timu maalum tayari imewekwa na KWS kukabiliana na visa vya aina hii haramu.

Wakati huohuo waendeshaji magari kwenye barabara za eneo hilo hasa Marula, Gilgil pa kupimia uzani na Soysambu wameonywa na kutakiwa kuwa waangalifu kufuatia idadi kubwa ya wanyamapori wanaovuka barabara kupata lishe.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...