Gavana Joho Akashifiwa Kwa Kulaani Mashambulizi ya Bamburi Akiwa Marekani

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 6 August 2019.

Gavana Joho Akashifiwa Kwa Kulaani Mashambulizi ya Bamburi Akiwa Marekani

Ali Hassan Joho, gavana wa Mombasa, ameshambuliwa vikali kwa kulaani shambulizi la Bamburi muda mfupi baada ya kupakia picha na video mtandaoni akijivinjari Marekani.

Shambulizi hilo lilisababisha majeraha mabaya kwa watu 13 na kuwaacha wakazi wa Bamburi, Bombolulu, na Kisimani wakipata shida.

Ali Hassan Joho alikilaani kisa hicho kupitia ukurasa wake wa Facebook na kutoa wito kwa maafisa wa polisi kuhakikisha washukiwa wanachukuliwa hatua kali za kisheria haraka iwezekanavyo.

"Nimesikitishwa sana na mashambulizi ya jana mtaani Bamburi na Mtopanga katika eneo la Kisauni. Natoa wito kwa maafisa wa polisi kuharakisha uchunguzi na kuwafungulia mashtaka wahusika wa shambulizi hilo," alisema Joho.

Ali Hassan Joho aliongeza kuwa ni jukumu letu kama serikali kuhakikishia wananchi usalama wa maisha na mali yao na kuwataka wananchi kujitolea kuwapa maafisa wa polisi taarifa zozote wanazojua kuwahusu shambulizi hilo.

Walakini, semi zake hazikupokelewa vyema na watu ambao walimkashifu kwa kuzungumzia usalama wa watu wa jimbo lake akiwa Marekani.

Idadi kubwa ya watu walihisi kwamba semi za Joho ni kama kejeli kwa wakazi wa Mombasa ambao walimpigia kura ikizingatiwa kwamba tukio hilo lilitokea saa chache baada yake kupakia video mtandaoni akijivinjari na Paris Hilton.

Shambulizi hilo limehusishwa na genge la Wakali Kwanza ambalo inasemkana limeanza kuwasajili vijana wa kujiunga nao.

Maafisa wa polisi wameimarisha usalama, lakini wasiwasi ingali imetanda katika maeneo hayo huku baadhi ya wakazi wakihofia kuwa hali ikawa mbovu zaidi.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...