This archive report was first published on 5 August 2019.
Makosa ya Mazoea Katika Matumizi ya Kiswahili ¶
Leo katika makala yetu ya Mwanga wa Kiswahili, tunaendelea kuangalia makosa ambayo watumiaji au wazungumzaji wa Kiswahili hufanya kwa kutojua au kufikiri kuwa ni sanifu au inakubalika.
Wakati wa kuunda nomino zinazotokana na mtendaji wa jambo fulani, makosa haya hujitokeza. Kwa mfano, wakati wa kuunda nomino za mtendaji, watumiaji wa Kiswahili hufanya makosa kama vile kutumia neno sharti lisipoteze maana na mantiki yake.
Kitenzi - nomino - makosa - sanifu/sahihi
- Leo mlindaji/mlindi mlinzi
- Jenga mjengaji/mjengi mjenzi
- Ongea muongeaji/muongezi mwongeaji
- Lima mlimaji/mlimi mkulima
- La mkulaji/mlaji
- Andika mwandikaji/mwandishi
- Pika mpiki/mpikaji mpishi
- Lea mleaji/mlezi
- Tembea mtembea/mtembeaji
- Vua mvuzi/mvuaji mvuvi
- Ja mkujaji/mjaji
- Tenda mtendi/mtendaji
- Ongea mwongeleleshaji/mwongeleshaji
Yapo makosa mengine hasa katika vitenzi vya silabi moja, kama vile fa, la, pa, ja, nywa, pwa, cha, nya, n.k. Vitenzi hivi hutatiza watu wanapotumia katika kuandika au kuzungumza.
Watu wengi hupenda kuongeza ku ili kuleta maana inayokusudiwa. Mifano ni kama; Kula mfano katika sentensi; Kula kwake/kwenu/kwao kunaudhi watu.
Kitenzi cha makosa ni kukula mfano; Kukula/kwake/kwenu/kwao kunaudhi watu.
Na mifano mingine ni kama; kukunywa badala kunywa, kukufa badala ya kufa, kukupa badala ya kupa, kukuja badala ya kuja.
Maneno haya hutumiwa ndivyo sana na watu katika mazungumzo na hata kuandika.
Tutaendelea kuaona na kunyoshana katika makala yetu wiki ijayo majaliwa.
Kumbuka Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie.
— Titus Sakwa – mwalimu, mchanganuzi na mwandishi wa Kiswahili.