Kanisa Lashtumu Mwimbaji Aliyenengua Kiuno Kwa Njia Ya 'Kuwapa Washirika Tamaa'

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 4 August 2019.

August 4, 2019, ilikuwa siku ya kushangaa kwa wanaoendesha kwaya ya kanisa maarufu nchini Nigeria baada ya mshirika mmoja kuonywa kwa kunengua kiuno chake kwa njia ambayo viongozi wa kanisa wanahisi si ya kumpa Mungu sifa.

Wakuu wa kwaya hiyo walimwandikia barua na kumpa masharti ambayo alitakiwa kufuata, kwa kuwa alikuwa akitumia mbinu ambayo inaweka wengine kuwa na tamaa.

Wakati wa kumtukuza Mungu, wanaoshiriki kwaya ya 'Praise and worship' huwa ni watu wenye vipawa vya kipekee, kama vile sauti nyororo ambayo huguza roho za washirika sawa na kuwa na viuno vyembamba vinavyojipinda wakati wa kucheza densi za kumtukuza Mungu.

Barua ilisema, 'Kamati ya nidhamu ya kwaya ya kanisa hili inakuandikia kukupa onyo kuhusu mtindo wako wa kupiga densi kanisani haswa wakati wa kumtukuza Mwenyezi Mungu.'

Wengi walishangaa kuhusu mtindo aliokuwa akitumia mwanachama huyo kiwango cha kufanya uongozi wa kwaya kumwandikia barua.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...