This archive report was first published on 4 August 2019.
Gavana Sonko na Millie Odhiambo Watoana Kwa Cheche ¶
Gavana wa Nairobi Mike Sonko na mbunge wa Mbita Millie Odhiambo waliangamia kwa cheche baada ya kutofautiana kuhusu hatua ya gavana kusema Ken Okoth alikuwa na mpango wa kando.
Utata ulianza wakati ambapo Sonko aliamka na kuamua kuwakemea Odhiambo pamoja na seneta mteule Isaac Mwaura baada ya kumkosoa kutokana na mazungumzo yake wakati wa hafla ya kumuomboleza aliyekuwa mbunge wa Kibra Ken Okoth.
Millie Odhiambo alisema Sonko ni mtu wa kupayuka kwenye matanga ovyo huku Sonko akipumua moto huku akitoa maneno ya nyuma ya pazia dhidi ya mbunge huyo.
Millie Odhiambo alidai kuwa Sonko tu hupiga domo kwenye mazishi badala ya kushughulikia sheria ambazo zitasaidia mambo ambayo anazungumzia.
Millie Odhiambo alisema, "Tofauti na wewe, mimi huwa siongei tu kwenye mazishi. Mimi hupitisha sheria ili kuwalinda watoto akiwemo huyo aliyezaliwa na Ken Okoth,".
Millie Odhiambo aligusa swala la Gavana Sonko 'kukosa baraka muhimu' na kuwahusu wawili hao.
Millie Odhiambo alisema, "Kile ambacho ninakijua, wanaume ambao hupenda kuwadhalilishi wanawake huwa ni wadogo sana pale chini,".
Utata uliongezeka na kuwa ya kudhalilishana huku wawili hao wakizungumzia hata maswala ya nyuma ya pazia.