This archive report was first published on 2 August 2019.
Mtoto wa miaka 7 wa India alikuwa na shida kubwa kwa sababu ya meno 526 kwenye ufizi wake, kulingana na taarifa kutoka kwa madaktari waliofanyia upasuaji.
Mtoto huyo alikuwa amelazwa hospitalini mwezi Julai baada ya kudai alikuwa akihisi maumivu kwenye ufizi wake wa chini.
Madaktari walimfanyia skana na walichopata kiliweza kuwaduwaza kwani mtoto huyo kando na meno 32 alikuwa na meno mengine 526.
Uvimbe huo kwa jina odontoma, ulikuwa ukitatiza meno yake kutomea kama kawaida.
Punde uvimbe huo ulipogunduliwa, madaktari hao walichukua hatua ya haraka ya kumfanyia upasuaji na kutoa meno hayo kwenye ufizi wake wa chini.
Odontoma ni uvimbe ambao hauwezi kusababisha saratani na pia ni aina ya magojwa ya meno ya hamartoma.
Hamartoma ni hali ambayo seli tofauti hukutana na kuanza kuoata katika sehemu fulani ya mwili hususan ufizi wa chini.
Mmoja wa madaktari aliyemfanyia mtoto huyo upasuaji alisema, "Kulikuwa na jumla ya meno 526 kuanzia milimita 0.1 (inchi 0.4) hadi milimita 15 (inchi 0.6). Kipande kidogo pia kilikuwa na mizizi ya kuonyesha ilikuwa jino."
Mvulana huyo aliondoka hospitalini baada ya kulazwa kwa siku tatu na anatazamiwa kupona.