Kipusa wa Kanyaike, Embu, Aachwa Mataani Kwa Kuanika Sira za Mchumba Wake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 2 August 2019.

Alhamisi, kipusa wa eneo la Kanyaike, kaunti ya Embu, alishindwa kudhibiti mdomo wake baada ya kutemwa na jamaa wake kwa kuanika siri zao kwa mamake.

Wawili hao walikuwa wameanza uhusiano wa mapenzi miezi mitatu pale ambapo jamaa alimfichulia mwanadada kuhusu biashara alizokuwa nazo.

Wakati wa kujadiliwa, kipusa alipewa mahari na akamfichulia mamake kuhusu mali ya jamaa, akimtaka ajipange kuitisha donge nono.

"Mama nimeona nikuchanue kwa sababu nimeangukia sonko. Ujipange wakati wa kuitisha mahari ili upate donge," kidosho alimnong'oneza mamake.

Alama ya mamake kusikia hivyo, alingiwa na tamaa na kuamua kumpigia simu jamaa akimpongeza kwa kumchumbia bintiye.

Walakini, jamaa alipokea habari hiyo, aliingiwa na hasira na akamtema kipusa papo hapo na kumsuta kwa kuwa domo kaya.

"Inaonesha utaendelea kumwaga siri zetu," jamaa alifoka.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...