Kontena la Zawadi Kutoka China Kwa Bunge la Kenya Lilifika Likiniwa Tupu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 2 August 2019.

Kontena la Zawadi Kutoka China Kwa Bunge la Kenya Lilifika Likiniwa Tupu

Waraka ulioandikwa Jumatano, Julai 31 kutoka kwa karani wa bunge Michael Sialai, ulithiitisha kuwa, kontena hilo lilifika Jumanne lakini lilipofunguliwa lilikuwa tupu.

Waraka huo ulisema kwamba, zawadi hiyo ilikuwa ni kutoka kwa China baada ya ziara ya Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya sasa ya National People’s Congress na maafisa wengine jijini Nairobi mnamo Aprili 13.

Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China ulisema ulishangazwa sana na tukio hilo ikitiliwa maanani kuwa, haijawahi kuwatokea hivyo popote.

Ubalozi huyo alisema, "Kwa miaka mingi serikali ya China imetoa msaada wa kirafiki kwa ndugu zetu Wakenya, vifaa vya matibabu, samani ya ofisini, chakula cha msaada, nk, na vyote vimekuwa vikifika salama. Miongoni mwazo ni vifaa vya ofisini vilivyoletwa Bungeni 2018. Kwa hivyo hii ni mara ya kwanza kwa tukio la aina hii,".

Ubalozi wa China amesema imani katika serikali ya Kenya kutatua suala hilo kikamilifu.

Idara ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) imeanzisha uchunguzi ili kujua ni jinsi gani kontena lililotarajiwa kuwa na vifaa kutoka China ambavyo ni zawadi kwa Bunge la Kitaifa lilifika Nairobi likiniwa tupu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...