This archive report was first published on 1 August 2019.
Wakati wa kujifunza umri wa kuoa, rafiki yao alikuwa hajaonesha dalili ya kuoa wala kuchumbiana na mwanadada yeyote.
Marafiki zake walikuwa wamechoka kumlisha kwani alikuwa na mazoea ya kuwatembelea kila jioni wakati chakula kilikuwa kinatayarishwa kabla ya kurejea kwake kulala baada ya kula.
Walipomuarifu kuhusu mpango wao kalameni aliwaambia kuwa alikuwa hajashindwa kujisakia bibi.
"Mimi sijashindwa kutafuta mke. Kwani mna shida gani?" polo aliwafokea wenzake.
Walishikilia kwamba walikuwa na nia nzuri katika uamuzi wao kwani hawakufurahishwa na jinsi alivyokuwa akiishi maisha yake.
Walipofanya uchunguzi, walibaini mwenzao alikuwa mwoga na hangeweza kuwarushia wanadada mistari.
Source: Tuko.co.ke