Mbunge wa Manyatta John Muchiri aomba msamaha baada ya kushambuliwa mitandaoni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 1 August 2019.

Mbunge wa Manyatta John Muchiri amelazimika kuomba msamaha baada ya kushambuliwa mitandaoni kwa kutundika picha yake kwenye mabasi ya shule ambayo yamefadhiliwa na pesa za maendeleo ya maeneo bunge.

Aliingiliwa na baadhi ya Wakenya mnamo Jumatano, Julai 31, ambao walimsuta kwa matumizi mabaya ya mamlaka.

Alijitetea na kusema kwamba alitundika picha zake kwenye basi hilo kwa ajili ya sherehe ya kuikabidhi shule ya upili ya Mtakatifu Benedict ya eneo la Kithimu.

Samahani kwa wale wote ambao wamechukizwa lakini nina basi zingine tano ambazo nitakuwa nikizikabidhi kwa shule mbali mbali. Mabasi hayo yametundikwa picha zangu ila zitaondolewa baada ya sherehe hiyo kukamilika. Nashukuru kwa maoni yenu kuhusu miradi yangu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...