This archive report was first published on 1 August 2019.
Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amesema anaunga mkono mswada wa uhalalishaji wa bangi kwa minajili ya dawa. Hii ni kwa heshima ya marehemu Ken Okoth ambaye alikuwa amewasilishwa mswada huo bungeni mwaka 2018.
Alisema hii wakati wa ibada ya wafu kwa mwendazake, na kuwataka wabunge ambao bado ni vijana kama Babu Owino na Charles Njagua (Jaguar) kusimama kidete na kuhakikisha kwamba mswada huo unaidhinishwa.
Madai ya Sonko yanajiri siku moja tu baada ya mwakilishi wa wanawake wa Nairobi Esther Passaris pia kutangaza kupitia mtandao wa Twitter kuwa anaunga mkono uhalalishaji wa bangi.