Gavana Waititu Afanikiwa Kulipa Dhamana ya KSh 15 Milioni Baada ya Kuzuiliwa kwa Siku Nne

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 1 August 2019.

Gavana Waititu Afanikiwa Kulipa Dhamana ya KSh 15 Milioni Baada ya Kuzuiliwa kwa Siku Nne

Agosti 1, 2019 - Gavana Ferdinand Waititu alilipa dhamana ya KSh 15 milioni baada ya kuzuiliwa kwa siku nne kwa madai ya ufisadi.

Waititu na mkewe Susan Wangari walijisalimisha kwa maafisa wa polisi Jumapili, Julai 28, ambapo walizuiliwa na kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani siku iliyofuata.

Mahakama ya kupambana na ufisadi iliamuru wawili hao walipe Ksh 19 milioni kabla ya kuachiliwa, lakini walishindwa kulipa pesa hizo mnamo Jumatatu, Julai 29.

Waititu alitakiwa alipe KSh 15 milioni huku Susan akiagizwa alipe KSh 4 milioni.

Washukiwa waliiomba mahakama kurejelea masharti hayo na kuwapunguzia dhamana hiyo, lakini ombi lao lilikataliwa.

Mkewe gavana alifanikiwa kulipa pesa hizo na akaachiliwa kutoka gereza la wanawake la Lang'ata.

Wawili hao walishtakiwa pamoja na washukiwa wengine 11 ambao inaaminika kwamba waliitapeli kaunti KSh 588,198, 328 zilizopaswa kutumika katika ujenzi wa barabara kwa na kuzipa kampuni zinazohusika na Waititu kandarasi pasi na kufuata utaratibu.

Kandarasi hizo zilipewa kwa kampuni M/S Testimony Enterprises Ltd ambapo wakurugenzi wa kampuni wanaaminika kuwa marafiki wa karibu wa Waititu, jambo ambalo maafisa wa kaunti walilifahamu.

Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 26.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...