Mhubiri Aliyekisiwa Kuwa 'Yesu' Kwa Muda Mrefu Kwa Watu wa Kitengela

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 31 July 2019.

Mhubiri Aliyekisiwa Kuwa 'Yesu' Kwa Muda Mrefu Kwa Watu wa Kitengela

Mnamo Jumatano, Julai 24, 2019, mtaa wa Kitengela ulikuwa na furaha tele pamoja na nderemo huku mzungu aliyekuwa amevalia mavazi ya kidini akipita.

Michael Job, mhubiri kutoka Marekani, alikuwa amevalia mavazi yake ya kuigiza huku akiwa amewachilia nywele zake.

Imeibuka kuwa Job ni muigizaji, mwinjilisti, na pia mkuu wa kanisa la Jesus Loves You Evangelistic Ministries.

Job alikuwa miongoni mwa wahubiri walioalikwa kuidhinisha misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo kwa jina Kiserian Mega Interdenominational.

Hafla hiyo ilifanyika kwa kipindi cha siku tatu ambapo 'Yesu' alizuru mashule na maboma ya watu.

Badala ya kuendesha punda, alikuwa akitimbelea kwa gari la kifahari akiwa chini ya ulinzi mkali huku akiwatazama wakazi hao wenye furaha akiwa juu ya gari.

Job anapenda kusafiri sana na kukutana na watu wa tabaka mbali mbali.

Michael Job alifanya ziara kwa mashule ambapo alipata nafasi ya kusifu pamoja nao.

Hafla hiyo ya madhehebu mbali mbali iliandaliwa kwa kipindi cha siku tatu.

Badala ya kutembea kwa punda mhubiri huyo alitumia gari la kifahari.

Job alikuwa miongoni wa mapasta waliikuwa wamealikwa kuzungumza katika hafla hiyo.

Michael Job wakati akihubiri katika hafla hiyo ya kikristu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...