This archive report was first published on 31 July 2019.
Wimbo wa Sailors, Wamlambez na Wamnyonyez, ulikuwa unapuuuzwa mwanzoni, lakini sasa umetazamwa na milioni mbili kwenye mtandao.
Wimbo huo ulianza kama wimbo wa kundi la wanamziki wachanga la Sailors, lakini sasa umefikia mpaka Marekani, ambapo muigizaji maarufu Jamie Foxx sasa ni mmoja wa wale ambao wanaangusha semi hizo kimtindo.
Alipomwambia Foxx atamke Wamlambez, ulimi haukuteleza, na Foxx alisema alifurahia kujifunza maneno ya kiswahili kama vile Wamnyonyez na Warembo wa Kenya.
Wimbo huo umetazamwa na zaidi ya watu milioni mbili kwenye mtandao, na kunaonekana kuwa kundi la Sailors lilijua kitu ambacho wengi hawakujua; mnato wa maneno hayo na labda hata mvuto kiseikolojia kutokana na maana yake fiche.