Neymar Jr: Kesi ya Ubakaji Imefutiliwa Mbali Kwa Ushahidi Usiofaa

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 30 July 2019.

Neymar Jr: Kesi ya Ubakaji Imefutiliwa Mbali Kwa Ushahidi Usiofaa

Maafisa wa polisi kutoka Sao Paolo, Brazil, wamewasilisha kesi ya ubakaji dhidi ya Neymar Jr, mchezaji wa Paris Saint-Germain, baada ya kukosekana kwa ushahidi.

Maafisa hao wamewasilisha kesi hiyo kwa waendesha mashitaka ili kufanya uamuzi wao wa mwisho katika kipindi cha siku 15.

Maafisa wa usalama kutoka nchini Brazil, wanasemekana kufutilia mbali kesi ya ubakaji dhidi ya nyota wa Paris Saint Germain, Neymar, kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

Madai ya ubakaji yalitokea wakati Neymar alituhumiwa na mwanamitindo wa Brazil, Najila Trindade, ambaye alidai kuwa Neymar alimlaza kikao wakati alimtembelea jijini Paris msimu uliopita.

Trindade alitumia mahojiano yake na televisheni moja nchini humo kufichua video iliyokuwa ikiwaonesha wawili wakitofautiana vikali hotelini.

Polisi walimkashifu Trindade kwa kumchafulia staa huyo wa soka jina na kumfungulia mashataka lakini akageuka tena kwa kuanza kudai kuwa maafisa hao walikuwa wafisadi.

Ofisi ya mwanasheria wa São Paulo, imethibitisha kuwa kesi hiyo imefutiliwa mbali lakini imewaruhusu waendesha mashtaka kutoa uamuzi wao wa mwisho.

Waendeshaji hao wa mashtaka watatoa uamuzi baada ya siku 15 kabla ya jaji kutoa uamuzi wake wa mwisho.

Maafisa wa Neymar, wanasema kuwa hakuwa tayari kuzungumzia uamuzi wa polisi.

Chapisho la AFP, linasema kuwa kesi hiyo imekuwa ikigonga vichwa vya habari vya magazeti nchini Brazil.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...