This archive report was first published on 30 July 2019.
Maajuzi ya Julai 30, 2019, jamaa wa eneo la Belgut, kaunti ya Kericho, alipokea habari kuhusu mke wake kuzaa mtoto wa kiume kabla ya kuoana na yeye.
Alipewa simu kutoka kwa shemeji yake aliyemtaka ajiandae kwani kulikuwa na sherehe ya jandoni ya mwanawe, kulingana na ripoti ya Taifa Leo.
Alipokea ushauri kwamba mkewe alikuwa amezaa akiwa angali shule ya upili na kwamba kwa kuwa babake mtoto huyo hajulikani, itamlazimu amgharamikie kama mzazi wake.
Ufichuzi huo ulimchoma sana jamaa ambaye alifululiza hadi nyumbani ili kubaini ukweli kutoka kwa mkewe.
"Kumbe tayari ulikuwa mzazi tukichumbiana? Ndoa hii itaporomoka leo nikigundua kwamba yale niliambiwa ni kweli," jamaa aliwaka.
Alipata fahamu na akaanza kupewa ushauri moja kwa moja baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza.