Gavana Waititu aachiliwa huru kwa dhamana ya KSh 15M na masharti mazito ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 30 July 2019.

Magazeti ya Kenya Jumanne, Julai 30, 2019: Gavana Waititu aachiliwa huru kwa dhamana ya KSh 15 milioni pesa taslimu, lakini dhamana hiyo pia inaandamana na masharti.

Wakati wa kuachiliwa huru, Waititu hatoruhusiwa kukaribia wala kuingia katika ofisi za Kaunti ya Kiambu wala kuwasiliana na mashahidi. Pia ametakiwa kuwasilisha stakabadhi zake za kusafiria nje ya nchi kortini.

Wakati huohuo, mahakama imemwachilia huru mke wa gavana huyo kwa dhamana ya KSh 4 milioni huku maafisa wengine walioshtakiwa na wawili hao kuhusiana na madai ya ufisadi wakipewa dhamana ya KSh 1 milioni kila mmoja.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...