Gavana Waititu na Mkewe Watalala Seli Tena Baada ya Mahakama Kukosa Kuamua Kuhusu Kuwachiliwa Kwa Bondi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 29 July 2019.

Julai 29, 2019 - Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na mkewe Susan Ndung'u watalala seli tena baada ya mahakama kukosa kuamua kuhusu kuwachiliwa kwa bondi.

Wawili hao walifikishwa mbele ya mahakama ya Milimani walipokutana na jaji Lawrence Mugambi na kukataa mashtaka sita yakiwemo matumizi mabaya ya afisi.

Wawili hao wanawakilishwa na mwanasheria Tom Ojienda kwenye kesi hiyo huku akiitaka mahakama kuwaachilia huru.

"Susan Ndung’u hana pasipoti. Pasipoti yake ilipotea na kwa hivyo hawezi kusafiri nje ya Kenya akiachiliwa," Ojienda aliambia mahakama.

Wawili hao walijipata kwenye matatizo baada ya kiongozi wa mshtaka ya umma Noordin Haji kusema kuna ushahidi wa kutosha kuwashtaki kuhusiana na sakata ya tenda za biashara kwenye serikali ya Kaunti ya Kiambu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...