Mwanahabari aomba msaada wa fedha ili kutoa mwili wa mamake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 28 July 2019.

Familia ya mwanahabari Carolyn Agosa imewataka wasamaria wema kujitokeza ili kuisaidia kuchanga fedha zitakazotumia kulipa bili kubwa ya hospitali ya Mater hapa jijini Nairobi.

Mamake Agosa, Evaline Kaseyi Majani, aliaga dunia Jumatatu Julai 1, 2019, kutokana na ugonjwa wa saratani na alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Mater hapa jijini Nairobi.

Bili ya hospitali ilifika KSh 1,340,470, lakini familia imeweza kulipa KSh 748,800 pekee kufikia sasa.

Familia inawaomba wasamaria wema kutoa mchango wao kwa nambari ya Paybill - 240559 na Account Name - Carolyn Agosa.

Kulingana na Agosa, hospitali imesema haitaruhusiwa kuuchukuwa mwili wa mwendazake hadi itakapokamilisha kulipa deni hilo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...