This archive report was first published on 28 July 2019.
Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu amekamatwa Jumapili, Julai 28, na kufunguliwa kwa mashtaka ya uporaji wa mamilioni ya pesa za umma katika serikali ya kaunti hiyo.
Naibu Rais William Ruto alisema Jumapili, Julai 28, kuwa Waititu hawafai kuendelea kuhudumu kama kiongozi wa kaunti hiyo.
Wanasiasa wa mrengo wa Kieleweke walisema mashtaka yanayomkabili Waititu ni mazito sana na lazima ang'atuke uongozini.
"Watu wanashikwa wameiba mali ya umma... huko Kiambu huyo mtu ameshikwa lazima atoke mamlakani. Waititu lazima ajiuzulu," alisema mbunge mteule Maina Kamanda.
Waititu alikamatwa baada ya kujisalimisha kwa maafisa wa polisi Jumapili, Julai 28, baada ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuamrisha kukamatwa kwa Waititu.