Seneta Orengo Aahadi Kuwa Wakili wa DP Ruto iwapo Atapatikana Katika Sakata ya Mabwawa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 28 July 2019.

Seneta wa Siaya James Orengo ameahidi kumwakilisha mahakamani Naibu Rais William Ruto iwapo atahusishwa na sakata ya mabwawa ya Arror na Kimwarer.

Alipokagua Elgeyo Marakwet Jumamosi Julai 27, Orengo alimtaka Ruto kuelezea kwa upana alichomaanisha aliposema ni KSh 7 bilioni pekee za ujenzi wa mabwawa hayo zilizopotea wala sio KSh 63 bilioni kama inavyodaiwa.

Alisema wale waliohusishwa katika sakata hiyo, sharti wabebe msalaba wao ila sio kuwalaumu viongozi wengine.

"Ningependa Ruto aandikishe taarifa kuhusiana na mabwawa ya Arror na Kimwarer, nitamsaidia kuandikisha taarifa hiyo na pia kumwakilisha mahakamani," Orengo alisema.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...