Mke wa Timbwani Alichapisha Mume Kwa Kumuoa Kipusa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 25 July 2019.

Timbwani, Likoni, Mombasa: Mke wa eneo hilo alishuhudia sinema ya bure baada ya kumtishia mumewe alipogundua alikuwa na njama ya kumuoa mke wa pili.

Penyenye zinaarifu kwamba jamaa huyo na mkewe walihamia pwani ili kukwepa visirani vya mara kwa mara bara.

Maisha yao yalianza kunawiri na kupata mali baada ya biashara yao kunawiri.

Alhamisi, mama huyo alipata fununu kwamba mumewe alikuwa ameanza uhusiano wa kimapenzi na kipusa mmoja wa eneo hilo.

Alibaini kwamba ilikuwa kweli na hata jamaa alikuwa anapanga tayari kumuoa mwanadada huyo.

Alipata hasira na kuchana mavazi aliyokuwa amevaa na kuapa kumfunza mumewe adhabu ambayo ataikumbuka milele maishani.

Alingiwa na baridi na kukatiza ghafla uhusiano wa mapenzi na mipango ya kumuoa kidosho huyo kufuatia vitisho alivyopewa na mkewe.

Source: Tuko

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...