Mbunge Oscar Sudi adai Rais Kenyatta ameshindwa na kazi, amtaka ang'atuke mamlakani ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 24 July 2019.

Julai 24, 2019: Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amemshambulia vikali Rais Uhuru Kenyatta kwa cheche za maneno na kudai kwamba ana uwezo wa kuliongoza taifa vyema kumliko.

Alizungumza nyumbani kwake huko Kapseret, Sudi alidai kwamba Uhuru ameshinda na kazi na kumtaka kujiuzulu ili yeye (Sudi) aongoze nchi.

Shambulizi lake halikukomea hapo kwani alizidi kumsuta rais na hata kumtaka kumpa nafasi ya miezi mitatu katika wadhifa huo ndiposa alete mabadiliko nchini.

Alisema ni sarakasi tu za kisiasa zinazofanywa kwani maadui wa kisiasa wanashambuliana, kwa kujieleza kuhusu kukamatwa na kushtakiwa kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Henry Rotich.

Alitetea Rotich na kudai ametumiwa na kutemwa na vigogo wa kisiasa, huku akidai kwamba Uhuru ameshindwa kuwatumikia Wakenya anavyopaswa.

"Uhuru ameshindwa kuwatumikia Wakenya anavyopaswa. Napendekeza aondoke mamlakani na anipe muda wa miezi mitatu katika wadhifa wa urais. Tulimpigia kura na sasa anafanyia utani uhusiano wake na Ruto. Rotich ametumiwa na kisha kutupwa kama tishu," Sudi alisema.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...