Waziri Henry Rotich na Washukiwa Wenzake Wakamatwa na Kufikishwa Mahakamani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 23 July 2019.

Waziri wa Fedha Henry Rotich alikamatwa na makachero kutoka idara ya upelelezi, DCI Jumanne Julai 23, 2019, kuhusiana na sakata ya mabwawa ya Arror na Kimwarer.

Rotich, pamoja na katibu wake mkuu Kamau Thugge na washukiwa wengine, alikabiliwa na mashtaka 15 ya ufisadi ambayo alikana mbele ya mahakama.

Washukiwa waliachiliwa huru kwa bondi ya KSh 50 milioni kila mmoja pamoja au dhamana ya KSh 15 milioni pesa taslim, lakini walikana mashtaka dhidi yao na wameonywa dhidi ya kuwasiliana na shahidi yeyote la sio dhamana yao itafutiliwa mbali.

Maafisa wengine walioshtakiwa ni pamoja na Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...