This archive report was first published on 23 July 2019.
Julai 21, 2019, siku ya Jumapili, Hassan Kajoke, mshambulizi kutoka Malawi, alikuwa mchezaji bora katika ligi dhidi ya malimbukeni Karonga United TNM.
Mechi hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa Kamuzu, ilishuhidiwa Nyasa Big Bullets wakiwapachika wapinzani wao mabao 5-0, huku Kajoke akiibuka kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo.
Alitunukiwa kuku baada ya kuandikisha matokeo bora, na shabiki wake aliyemuomba ruhusa ili kumkabithi zawadi yake.
Shabiki huyo alihakakikisha kuwa kuku huyo ana rangi sawia na jezi waliokuwa wamevalia mabingwa hao wa Super Ligi.
Clubs hiyo ilianika picha ya Kajoke akipokea kuku huyo kwenye mtandao wao wa Facebook, na kuibua hisia mseto mtandaoni.