This archive report was first published on 23 July 2019.
Sonko na Passaris Wameelekea Kuridhiana Tenan ¶
Gavana wa Nairobi Mike Sonko na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti hiyo Esther Passaris wameelekea kuridhiana tena baada ya kuvuana nguo hadharani Juni 1.
Waliandamana na Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya uzinduzi upya wa Kiwanda cha Kampuni ya Maziwa ya KCC, Mowlem, Dandora, Nairobi, Jumamosi, Julai 20.
Wakiwa kwenye uzinduzi huo, Sonko na Passaris walionekana wakishiriki mazungumzo bila ya kuoneana aibu, na mojawapo wa picha imeashiria kuwa, huenda wameridhiana hatimaye.
Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Masuala ya Jinsia ililazimia kutoa taarifa ikikashifu vikali ilichotaja kuwa mtindo mbaya wa baadhi ya viongozi kushambulia na kuwadunisha viongozi wanawake.
Wabunge wa kike wakiongozwa na Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo walimshutumu sana Sonko kwa kumkosea heshima Passaris.