Mama Kutoka Mwea Asutwa Kwa Kutaka Mabinti Zake Wawe na Masponsa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 23 July 2019.

Kitendo cha mama huyo kutoka eneo la Makima, Mwea kwa kuwashauri mabinti zake kutafuta masponsa kimegadhabisha wenzake kwa kiasi kikubwa.

Wenzake waligundua kwamba mama huyo alikuwa akiwashauri binti zake kuwapagawisha na kuwachota kimapenzi wazee ambao walikuwa na mali katika eneo hilo.

Wanawake hao waligadhabishwa pale ambapo binti mmoja wa mama huyo alipachikwa mimba na mzee mmoja na eneo hilo na kisha mamake kumshauri amkwamilie ndiposa amuoe.

Wakati wa kujadili hali hiyo, mwenyekiti wa kikundi hicho alimwambia mama huyo, "Badala ya kuwahimiza binti zako wawe na nidhamu unawahimiza wawe na masponsa. Hii haifai. Unajiaibisha."

Alama hii ya kujiaibisha ilisababisha mama huyo kujibu kwa kujiondoa na kuwataka wawache kuingilia masuala ya familia yake.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...