This archive report was first published on 22 July 2019.
Bwenyenye Simon Gicharu: Vijana Waliofuzu Vyuo Vikuu Wapewa Suri Ya Kuajiriwa Kazi ¶
Julai 22, 2019 - Bwenyenye Simon Gicharu, mwenyeji wa Chuo Kikuu cha Mt Kenya, amewapa ushauri vijana waliofuzu vyuo vikuu kuhakikisha kuwa wanapata ajira wakati huu ambapo wengi wanalia ukosefu wa kazi.
Simon Gicharu alisimulia jinsi alivyoweza kuwavutia watu mashuhuri kwenye ulingo wa biashara wakati alikuwa na umri wa miaka 29. Alisema alipokuwa na suti nzuri, alifika katika wizara ya masuala ya biashara na kutaka mkutano na waziri wa wakati huo Kirugi M'mukindia.
“Nilijiambia kuwa kile kibaya naweza kupata ni kukosa kupata nafasi ya kukutana naye. Nilishangaa wakati ambapo waziri alikumbali ombi langu,” Gicharu alisema.
Ushauri wa Bwenyenye Gicharu unajiri baada ya runinga moja humu nchini kuangazia taarifa ya mwanafunzi aliyefuzu chuo kikuu na shahada lakini amekuwa kalameni wa mtaani tu.
Wakenya wengi walianguka kwa taarifa ya Kelvin Ochieng, mwanafunzi aliyefuzu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na shahada lakini amekuwa kalameni wa mtaani tu.