This archive report was first published on 21 July 2019.
Julai 21, 2019 - Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu amesema kuwa mrengo wa kisiasa wa Kieleweke haumpigii debe Raila Odinga kwenye siasa za urais za 2022.
Alisema hilo wakati wa mkutano wa wabunge wa mrengo huo katika eneo la Githunguri na Kangema.
Wambugu alisema kuwa kampeni zao si za kisiasa, lakini ni kumsaidia Rais Uhuru Kenyatta aweze kutimiza malengo yake.
Alisema kuwa wataendelea kupigia debe mwafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, maarufu kama 'Handshake', ambayo inamwezesha rais kutekeleza mipango ya maendeleo.
Aliongeza kuwa wataendelea kupigia debe mwafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, maarufu kama 'Handshake', ambayo inamwezesha rais kutekeleza mipango ya maendeleo.
Wabunge wa mrengo wa Kieleweke katika mkutano wa hapo awali. Picha: Ngunjiri Wambugu