Wanasiasa wa Jubilee na ODM waingiwa na woga kuhusu Punguza Mzigo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 21 July 2019.

Mapendekezo ya mrengo wa Punguza Mzigo, yaliyotangulia IEBC kuwa na sahihi milioni moja, yamezingirishwa na wanasiasa wa Jubilee na ODM.

IEBC ilitangaza kuwa mrengo huo uliweza kufikisha sahihi milioni moja, na kwa hivyo mswada wake wa mageuzi utaanza kutumwa kwa mabunge ya kaunti ili kujadiliwa.

Wanasiasa wa Jubilee na ODM wamezungumza kuhusu mapendekezo haya, na wamezingiria kuunga mkono mswada huo.

Seneta wa Siaya James Orengo alisema kuwa hakukuwa na majadiliano mazuri kuhusu mswada huo wa Punguza Mzigo.

"Swali la mageuzi ya katiba ambalo linaletwa kwenye mabunge ya kaunti halikufanyiwa majadaliano mazuri," Orengo alisema.

Mbunge wa ODM Opiyo Wandayi vile vile alisema anapinga mapendekezo ya mrengo wa Aukot na kuwataka maMCAs kutoyaunga mkono.

"Napinga mapendekezo ya Ekuru Aukot. Lazima wasubiri kamati iliyoundwa na Uhuru na Raila kuchukua maoni kutoka kwa wananchi ili itoe mwelekeo wa referendum," Opiyo alisema.

Aden Duale, Kiongozi wa Wengi kwenye bunge, alisema kuwa wanasiasa wa Garissa watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuunga mkono mswada huo.

"Hutuko tayari kuunga mkono mageuzi ya katiba ambayo yanakusudia kutoa baadhi ya nafasi za uakilishi kwenye kaunti na maeneo bunge. Tutakabiliana vilivyo na yeyote hapa Garissa atakayejaribu kuunga mkono mswada huo," Duale alisema.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...