Sadio Mane atakuwa na wakati mgumu kujitayarisha kwa msimu mpya wa Liverpool

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 18 July 2019.

Sadio Mane atakuwa na wakati mgumu kujitayarisha kwa msimu mpya wa Liverpool

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kuwa Sadio Mane atakuwa na wakati mgumu kujitayarisha kwa msimu mpya wa Liverpool, kwa kuwa atashiriki katika mechi ya Senegal dhidi ya Algeria katika fainali ya AFCON mnamo Ijumaa, Julai 19.

Mane anatazamiwa kurefushiwa likizo yake kabla ya kujiunga na kikosi chake cha Liverpool kwa mashindano ya Community Shield dhidi ya Manchester City mwezi Agosti 4.

"Tutajua hisia zake Sadio, baada ya fainali. Itakuwa vigumu sana kwake siku 16 kabla ya kukutana na City, na msimu wake utakuwa umekamilika. Tutalazimika kufanya uamuzi ambao bado hatujaufanya," Klopp alinukuliwa akiambia Liverpoolfc.com.

Wachezaji hao walirefushiwa likizo yao baada ya kushiriki katika mtanange mkubwa za kimataifa huku Firmino na Alisson wakiinua kombe la Copa America na timu yao ya taifa ya Brazil, naye Salah akashindwa kuipa Misri ushind katika kipute cha AFCON.

"Ningetarajia warejee baada ya wiki moja lakini haingekuwa na maana! Kwa hivyo, walikuwa na likizo ya wiki tatu kisha tutakuwa nao hapa kabla ya msimu," Klopp alimalizia.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...