Katika chapisho la 20 Novemba 2018, Rachel amesema bado anatafuta upatanisho na aliyekuwa mume wake, Kenneth, lakini juhudi zake za kurejesha ndoa zimekuwa zikikwama kwa muda mrefu.
Rachel alisema yeye na Kenneth walitengana mwaka wa 2014, na kwamba tangu wakati huo wameendelea kuwasiliana. Hata hivyo, anadai kila anapomweleza kuhusu kurudiana kama mke na mume, Kenneth hukataa.
“Tunazungumza naye lakini ile ikifika kumwambia achukue hatua turudiane kama bibi na bwana huwa anakataa.” Alieleza bi Rachel.
Alisema chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wao kilikuwa wakati Kenneth alipoondoka na kumuacha nyumbani mtoto akiwa mgonjwa, kisha hakurudi tena. Wawili hao walikuwa wamejaliwa mtoto mmoja ambaye baadaye aliaga dunia.
Rachel pia alisema kuwa katika kipindi cha kutengana walipata mtoto mwingine, lakini bado Kenneth hajaonyesha nia ya kurudiana naye.
Kwa upande wake, Kenneth alikata simu mara tu Gidi alipojitambulisha, hatua iliyofunga mazungumzo hayo bila kupata msimamo wake kuhusu madai ya Rachel.
Pata uhondo kamili.