This archive report was first published on 29 June 2019.
Mnamo tarehe 29 Juni 2019, maafisa wa Idara ya Kuwalinda Wanyama Pori (KWS) waliwakamata wafanyabiashara 15 katika soko la Burma wakiwa na kilogramu 800 za nyama ya punda milia. Inaaminika kwamba nyama hiyo ilikuwa tayari imenza kuuziwa kwa wananchi.
Kulingana na taarifa ya KWS, maafisa hao walisema kwamba walianza kuwachunguza wafanyabiashara hao baada ya kuonekana wakiondoka na punda milia katika shamba la Portland Athi River, Machakos.
Maafisa wa KWS wakishirikiana na maafisa wa polisi walianza kuwafuata washukiwa hao ambao inaaminika wamekuwa wakishiriki uwindaji haramu. Gari lililokuwa likitumika katika usafirishaji wa nyama hiyo pia lilikamatwa.
Endapo washukiwa hao watapatikana na makosa ya uwindaji haramu na uuzaji wa nyama pori basi watafungwa jela kwa muda usiopungua miaka mitatu. Washukiwa watafikishwa mahakamani Jumamatu.