Skip to main content

Esther Arunga Kurushwa Jela Kwa Mauaji Ya Mwanawe

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 18 July 2019.

Esther Arunga Kurushwa Jela Kwa Mauaji Ya Mwanawe

Esther Arunga, mtangazaji wa zamani wa KTN TV, amekurushwa jela kwa miezi 10 kwa mauaji ya mwanawe, Sinclair, aliyeaga dunia 2014. Hukumu ilifanywa na Mahakama ya Juu Zaidi ya Brisbane.

Arunga alikabidhiwa jela kwa miezi 10, lakini akamwachiliwa huru baada ya kukubali masharti fulani kabla ya muda wake gerezani kukamilika.

Alitishwa jela kwa kuficha ukweli kuhusu kifo cha mwanawe, na kwa kuwadanganya polisi kuhusiana na kifo hicho.

Alipokamatwa, Arunga alisema kuwa Sinclair alikuwa ameanguka na kubingiria kwenye ngazi ya kupandia, lakini baadaye alibadilisha kauli yake na kuwaeleza polisi kwamba ni mumewe aliyempiga ngumi ya tumbo mwanawe.

Maafisa kutoka huduma za dharura walitoa ushahidi wao na kuelezea hali ilivyokuwa walipofika eneo la tukio nyumbani kwao Kallangur, Brisbane na kuupata mwili wa Sinclair.

Jaji Martin Burns alinukuliwa na Associated Press la Australia akisema kuwa, aliionea huruma hali yake Arunga alipozungumza na polisi waliokuwa wakichunguza kifocha mwanawe.

"Huenda ulikuwa katika hali ya mshtuko kwa kifo cha mwanao, wakati ukihojiwa... na vilevile kuomboleza," alisema Jaji Burns.

Alisema imani za tamaduni zilichangia pakubwa na kwamba alipitia hali ngumu kipindi cha miaka mitano tangu kutokea kisa hicho.

"Hali ilibadilika kutoka kwa mke na mama, ambaye wakati huo alikuwa akinyonyesha mtoto wa miezi sita, na aliyekuwa akijaribu kuijenga familia katika nchi geni, hadi kumpoteza mtoto, mume na binti zako," aliongeza Jaji Burns.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →