Kitendo cha KNEC kwa kuchagua mtihani wa Gredi ya 6 wa CBC na majibu ya kuchagua kama ilivyo KCPE, kuna wasiwasi kwamba mtihani huu hauna tofauti kubwa na KCPE.
Kitendo hiki kinaonekana kuwa kinyume na jinsi ilivyokuwa ikitoa mitihani yake ya hapo awali ambapo ilimhitaji mwanafunzi kufikiria jibu na kuliandika moja kwa moja katika mapengo yaliyoachwa wazi.
Ingawa KNEC inasema kuwa alama za mwisho za mwanafunzi zitakuwa ni jumla ya mitihani aliyofanya mwanafunzi katika Gredi ya 4, 5 na 6, kuna hofu kuwa kuna wanafunzi wengi sana wasiokuwa na alama hizo kutokana na changamoto za kuwasilisha alama hizo kwa KNEC na pia walimu wengi kukosa ufahamu wa vile walivyostahili kufanya.
Kitendo cha KNEC kwa kuchagua mtihani wa Gredi ya 6 wa CBC na majibu ya kuchagua kama ilivyo KCPE, kuna wasiwasi kwamba mtihani huu hauna tofauti kubwa na KCPE.