Umaskini wafaidi kampeni za vigogo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Umaskini wafaidi kampeni za vigogo

Na Collins Omulo

Naibu Rais William Ruto na mwanaurais wa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga wameanza kutumia suala la umaskini kusaka kura kwa ahadi kuwa watasaidia walalahoi wakishinda.

Wataalamu wa uchumi wanasema ahadi za wawili hao kukabiliana na hali mbaya ya uchumi nchini ni mbinu tu ya kujitafutia kura kwani hawaelezi mbinu watakazotumia kutekeleza ahadi hizo.

Wanasiasa hao wanatumia umaskini na matatizo ya uchumi katika kampeni zao kutokana na kutambua mahangaiko wanayopitia wengi kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa, ukosefu wa ajira, mfumo wa afya ulioporomoka, ukame miongoni mwa matatizo mengine tele.

Mapema Mei, kura ya maoni iliyothaminiwa na kampuni ya Nation Media Group ilionyesha kuwa asilimia 75 ya Wakenya wana hofu zaidi kuhusu gharama ya juu ya maisha.

Idadi ya watu maskini nchini imeongezeka maradufu tangu 2014 huku matajiri wakitajirika zaidi na maskini wakizama zaidi katika uchochole, hivi kwamba kuna watu wawili ambao mali yao inatoshana na ya maskini milioni 16 wakiwa wamejumuishwa.

Naibu Rais William Ruto na mwanaurais wa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga wamechukua fursa ya hali hiyo kubuni mikakati ya kampeni zao wakiwa na lengo la kushawishi wanyonge kuwaunga mkono.

Next read

Meru Residents vs State Machinery: Inside Fierce Battle to Grab Kirimancuma Primary School Land as Rogue Officials Ignore High Court Orders

8 August 2026 · 8 min read

A fierce land dispute unfolds in Meru as residents challenge attempts to excise Kirimancuma Primary School land despite court orders.