Walimu Wataka Vyumba Vya Kunyonyeshea Vijengwe Shuleni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Shule za umma bado hazijazingatia sheria ya 2016 inayotaka serikali kujenga vituo vya kunyonyeshea watoto shuleni.

Wizara ya elimu inahitajiwa kuanzishaa vituo hivyo katika taasisi zote za umma, lakini shule za umma bado hazijazingatia sheria hiyo.

Walimu wa kike hasa walio na watoto wachanga hulazimika kwenda nyumbani mara kwa mara shule zinapofunguliwa ili kunyonyesha na hivyo kupoteza wakati na pesa.

“Tunataka kusaidia walimu wanawake walio na watoto wachanga na wanaohisi haja ya kwenda nyumbani kuwanyonyesha,” alisisitiza Benta Opande, mkurugenzi wa Muungano wa Walimu Wanawake Nchini (Kewota).

Next read

Governor Natembeya's Vehicle Torched in Homa Bay as State Targets Experienced Opposition Politicians

18 August 2026 · 4 min read

"Natembeya's car was set ablaze and he was forced to flee through a fence as the state turns on experienced politicians, just days after...