Skip to main content

Gavana Alfred Mutua Akutana na Raila, Aashiria Kuundwa Kwa Chama Cha Kisiasa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 July 2019.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua alimtembelea Raila Odinga katika afisi yake ya Capitol Hill mnamo Jumatano, Julai 17, 2019, wakifanya mazungumzo kuhusu mambo kadhaa ikiwemo siasa za uchaguzi mkuu 2022.

Alfred Mutua, ambaye tayari ametangaza azma yake ya kuwania urais 2022, alifichua kwamba alimuomba Raila ushauri wa jinsi anaweza jizolea kura na pia iwapo angeshirikiana naye kuunda chama cha kisiasa.

Wawili hao walikubaliana kushirikiana ili kupigana na ufisadi na kuhakikisha kwamba viongozi wote ambao watahusishwa na donda ndugu hilo wanaadhibiwa vilivyo.

Alfred Mutua alisema kwamba walikubaliana na Raila nchi inahitaji kiongozi wa kuleta maendeleo ambaye anaweza pigana na ufisadi kwa ujasiri.

Wawili hao walikubaliana kuendelea kujadiliana mara kwa mara kuhusu mambo muhimu ambayo yanaathiri taifa.

Source: Tuko.co.ke

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →