Skip to main content

Joseph Hellon: Mumewe Esther Arunga alikuwa akitumia uchawi ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 July 2019.

Joseph Hellon, mhubiri wa Finger of God, amesema Quincy Timberlake, mumewe aliyekuwa mwanahabari Esther Arunga, alikuwa akitumia uchawi.

Timberlake na Arunga walikuwa washirika wa Hellon katika kanisa la Finger of God kabla ya wawili hao kuondoka nchini Kenya huku maisha yao kuzongwa na utata.

Julai 16, Hellon alisema katika mahojiano na NTV kwamba Timberlake alikuwa amempasulia mbarika kuwa alikuwa ni mchawi lakini alitaka kuingia kanisani ili aokolewe.

"Quincy alikuwa akitumia mbinu za uchawi... na ninajua hayo kwa sababu aliniambia," Hellon alisema.

Arunga alikutana na Timberlake kwenye kanisa la Hellon na penzi likaota kati yao.

Wapenzi hao wawili wanazidi kupitia matatizo mengi nchini Australia ambapo wana kesi ya mauaji ya mtoto wao.

Arunga alikiri kwa maafisa wa polisi kuwa alikuwa ametoa habari za uongo kuhusu kilimuua mtoto wao ili kumlinda mume wake.

Source: Tuko, Julai 17, 2019

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →