Skip to main content

Uganda: Mhubiri wa House of Prayer Ministries Aloysius Bugingo anasakwa na polisi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 16 July 2019.

Polisi nchini Uganda wamekaswa mhubiri wa House of Prayer Ministries Aloysius Bugingo siku chache tu baada ya kutoa matamshi ambayo wengi walihisi ni ya kudhalilisha mkewe.

Maafisa wa polisi walimtaka mhubiri huyo kuandikisha taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Alisema Jumatatu, Julai 15, Mkuu wa polisi mjini Kampala Patrick Onyango kwamba mhubiri huyo alitakikana kuandika ripoti kwani matamshi yake yalisababisha maandamano kutoka kwa wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu.

Onyango alisema, "Kamanda Moses Kafeero alimtaka mhubiri Bugingo kufika katika kituo cha polisi wazungumze ili wajue watakavyo suluhisha jambo hilo."

Maandamano hayo ya wanaharakati yalitibuliwa huku Daily Motion ikitangaza kuwa polisi walisema wanaharakati hao walikosa kufuata sheria.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →