Skip to main content

Filamu ya Subira kutoka Kenya yashinda tuzo mbili ZIFF 2019

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 14 July 2019.

Filamu ya Subira kutoka Kenya yashinda tuzo mbili ZIFF 2019

Usiku wa jana Julai 13, 2019, filamu ya Subira iliyotengenezwa kisiwa cha Lamu na Jiji la Nairobi nchini Kenya ilipata tuzo mbili kwenye tamasha la 22 la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka huu.

Wajaji wa tuzo hizi walielezea filamu hiyo kuwa ni ya mfano kati ya filamu zilizoingia kwenye kinyang'anyiro cha ushindi.

Wajaji walionaoa filamu hiyo ni mkufunzi wa masomo ya filamu na televisheni Bi. Lizzele Bisschoff kutoka Uingereza, Nadia Bulbulia (Afrika Kusini), Amina Peter, na Profesa Bi. Mette Hjort (Uchina).

Alisema Mhariri wa filamu hiyo Roselidah Taabu, "Filamu hizi zimetupatia heshima. Tunawaomba watu wa filamu wengine wakiwemo walio Kenya waweze kuitumia nafasi ya jukwaa la ZIFF kuwasilisha filamu zao."

Subira ni filamu ya mwaka 2018 inayomweleza Binti aitwaye Subira ambaye alikuwa na ndoto ya kujua kuzamia hii ilitokana na kuwa mara zote alienda na baba yake baharini kuvua lakini hakupata nafasi zaidi ya kumshuhudia tu baba yake akizamia huku yeye akibaki kwenye jahazi na hivyo kuwa na hamu ya kutaka kujua lakini baba yake aliyetoa ahadi ya kumfundisha ghafla anapata ajali baharini na kufa na hapo Subira kuingia kwenye misukosuko ikiwemo kuozeshwa wakati huku hakuwa tayari kwa hilo.

Alisema Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Waziri wa habari, Utalii na mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo, "Wadau wanahitajika zaidi katika kuendelea kudhamini kwa mwakani tena."

Alisema Mkurugenzi wa tamasha hilo, Bi. Firdouse Bulbulia, "Kwa mwaka huu tamasha hilo limedhaminiwa na Azam Media kupitia Azam TV huku pia likiwa na wadhamini wengine kama Zanlink, Global Education link, Zenjy water, Park Hyatt Hotel, Maru maru hotel, Zancinema, Print Plus, Memory of Zanzibar, SOS Children’s Villages Zanzibar, Beach House na wengine wengi."

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →