Skip to main content

Marekani: Wasiwasi waibuka baada ya Trump kutaka wahamiaji kufurushwa

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 14 July 2019.

Marekani: Wasiwasi waibuka baada ya Trump kutaka wahamiaji kufurushwa

Wasiwasi umetanda nchini Marekani baada ya Rais Donald Trump kutaka wahamiaji wote walio nchini humo kinyume cha sheria kufurushwa. Taarifa hii ilikuwa ni kati ya habari zilizotolewa na Rais Trump kwenye mtandao wa Twitter mnamo Jumamosi, Juni 22.

Trump alisema kuwa mrengo wa Democrats nchini Marekani ulimtaka aahirishe msako wa kuwafurusha wahamiaji walio nchini humo kinyume cha sheria kwa wiki mbili ili mrengo huo pamoja na ule wa Republicans watafute suluhu la swala hilo.

"Mrengo wa Democrats umenitaka niahirishe msako wa kuwafurusha wahamiaji walio nchini kinyume cha sheria kwa wiki mbili ili mrengo huo pamoja na ule wa Republicans watafute suluhu la swala hilo," Trump aliandika.

Maandamano ya kupinga msako huo wa wahamiaji wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria yamekuwa kwa siku nyingi tangu Ijumaa, Julai 12. Miji ambayo misako mikali inatarajiwa ni Atlanta, Baltimore, Chicago, Denver, Houston, Los Angeles, Miami, New Orleans, New York na San Francisco kulingana na taarifa za runinga ya NBC.

Trump alisisitiza kuwa wote walioingia nchini humo kinyume cha sheria hawana lingine ila kurudishwa katika nchi walizotoka.

Maafisa wa serikali kutoka idara ya uhamiaji wataanza kuwasaka wahamiaji wote walio nchini humo kinyume cha sheria kuanzia Jumapili, Julai 14.

Maandamano ya kupinga msako huo wa wahamiaji wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria yamekuwa kwa siku nyingi tangu Ijumaa, Julai 12.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →