Andrew Kibe: Mtangazaji mwenye utata afichua enzi zake wakati alijitolea kanisani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 13 July 2019.

Mtangazaji Andrew Kibe amefichua enzi zake wakati alikuwa amejitolea kumtumikia Mungu kanisani kabla ya kuwa 'mwana mpotevu' baada ya kupata kazi na redio ya NRG.

Kibe alifichua habari hii kwenye ujumbe wake wa Jumapili, Mei 5, 2019, kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mtangazaji huyo alishangaza mashabiki zake baada ya kufichua taswira kuhusu maisha yake ya kale ambayo inakinzana kabisa na mienendo yake ya sasa.

Kibe alisema, "Miaka michache iliyopoita, wakati kama huu, ningekuwa kanisani nikiimba na kumwabudu Mungu. Mambo hubadilika huh. Watu bado huenda kanisani ama nilisalia pekee yangu?"

Wafanyikazi wenzake ambao walikuwa karibu naye enzi zile walishuhudia kwamba alikuwa mkristo halisi na alikuwa mstari wa mbele katika maswala ya kanisa.

Kibe na mtangazaji mwenza Kamene Goro waliondoka NRG na inakisiwa kwamba wawili hao walikuwa wanaelekea katika kituo cha Kiss 100.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...