Seneta Orengo: Ruto Anapaswa Kuheshimu Uhuru

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 13 July 2019.

Seneta Orengo: Ruto Anapaswa Kuheshimu Uhuru

Seneta wa Siaya James Orengo amemtaka Naibu Rais William Ruto kukoma kuidharau serikali aliyounda, kwa kusema kwamba Ruto anapaswa kuheshimu Rais Uhuru.

Orengo alisema hili wakati wa uzinduzi wa miradi kadhaa katika eneo bunge la Rarieda, Siaya.

Alisema kwamba Ruto anapaswa kujua kwamba Uhuru ni Rais wa Jamhuri ya Kenya na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya jeshi.

"Ruto ni lazima kujua kuheshimu Kiongozi wa Taifa. Ruto pia ni lazima kufahamu Uhuru ni rais wa Jamhuri ya Kenya na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya jeshi. Ni lazima kufahamu Uhuru ni bosi wake," alisema Orengo.

Alisema hili wakati Orengo alikuwa akisimamia kura ya maamuzi inayotazamiwa kabla ya 2022, ambayo inatazamiwa kuleta msisimko mkali katika Upinzani na chama tawala.

Wanasiasa wanaotaka marekebisho wanasema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi ili kuwe na mapande matatu, lakini kambi ya Ruto inakataa kwa kiudai kuna njama ya kukandamiza upande wao.

Matamshi ya Orengo yanajiri wakati kukiwapo na madai ya mgawanyiko katika baraza la Mawaziri kufuatia madai ya kuwapo njama ya kumwangamiza naibu rais.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...