Skip to main content

Spishi Mpya ya Samaki Iliyogunduliwa, Yapewa Jina Wakanda

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 12 July 2019.

Julai 11, 2019, wanasayansi kutoka Shule ya Sayansi ya California waligundua spishi mpya ya samaki mwenye rangi dhahiri, iliyopewa jina Wakanda.

Samaki huyo, wenye urefu wa 6cm, aligunduliwa katika maeneo ya matumbawe chini ya bahari 200ft katika pwani ya Zanzibar, Tanzania.

Wanasayansi hao walipata samaki huyo wakati wa utafiti wao wa kuzama baharini, na kuwakumbusha mavazi ya Black Panther katika filamu hiyo ya uhalisia ajabu.

"Tulipofikiria kuhusu maisha ya siri ya mawe ya chini baharini ambayo hayajafikiwa na mtu, tulifahamu ni tulistahili kuita aina hii ya spishi Wakanda," alisema Yi-Kai Tea, Taxonomist kutoka Chuo Kikuu cha Sydney, Australia.

Spishi hiyo ya samaki inaungana na spishi nyingine saba katika maeneo ya magharibi mwa Bahari Hindi, huku jamaa za samaki hao wakisambaa hadi Bahari ya Pacific.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →