Skip to main content

Wafanyabiashara wa City Market wamemsihi Inspekta Hillary Mutyambai kuwalinda dhidi ya wachuuzi wa mitaani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 12 July 2019.

Wafanyabiashara wa City Market wamemsihi Inspekta Hillary Mutyambai kuwalinda dhidi ya wachuuzi wa mitaani ambao wamedai wanawatishia maisha.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Cyrus Kamundia, wafanyabiashara hao wamesema kwamba wamekuwa wakipokea jumbe kutoka kwa wahuni ambao wamekuwa wakiwatishia kwa shinikizo lao la kuwataka wachuuzi kuzuiwa kufanyia biashara katika soko hilo.

Wafanyabiashara hao walisema kwamba sio haki kwa wamikili wa maduka hayo kufanya kazi pamoja na wachuuzi hao ambao hawalipi ada ya leseni katika jengo la City Hall.

Wafanyabiashara hao walisema kwamba wachuuzi hao wanaokoa pesa kwa kiasi kidogo, KSh 50 pekee, huku wenyewe wanaokoa KSh 100,000 kila mwaka ili kugharamia leseni, umeme, ukaguzi wa afya miongoni mwa mengine.

Wafanyabiashara hao walisema kwamba wana hitaji la kupewa usalama haraka iwezekanavyo kutoka kwa afisi ya IG ili kuhakikisha maisha yao yamehifadhiwa.

Wafanyabiashara hao walisema kwamba wanaomba serikali ya kaunti kuwapa kipande cha ardhi wachuuzi hao kando na eneo hilo ili kusitisha uhasama wa kibiashara baina yao.

Maisha ya wafanyabiashara hao yamo hatarini na wanahitaji kupewa usalama haraka iwezekanavyo kutoka kwa afisi ya IG.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →