Ferdinand Omanyala Asks Government to Waive Fees at Top Sports Facilities

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Bingwa wa mbio za mita 100 nchini, Ferdinand Omanyala, ameiomba serikali kuondoa ada za juu katika viwanja vya michezo ili kukuza vipaji vya wanamichezo.

Amesema ada za juu zinazotozwa ili wanamichezo waruhusiwe kutumia majukwaa ya michezo Kenya, zinazima ndoto za baadhi wasio na uwezo kifedha lakini wangependa kupalilia talanta zao.

“Ukizuru viwanja vya serikali vyenye vifaa bora vya kufanya mazoezi, ni lazima ulipie. Kikwazo cha uwanja kinazima ndoto za vijana wengi waliojaaliwa vipaji mbalimbali katika michezo,” Omanyala alisema.

Alitoa kauli hiyo siku chache baada ya kung'aa katika awamu ya tatu ya mashindano ya Athletics Kenya uwanjani Nyayo, Nairobi.

Alisema ukosefu wa uwanja bora kufanya mazoezi ulimhangaisha, na kuwahimiza serikali kuondoa ada za juu katika viwanja vya michezo.

Alitaja uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa MISC Kasarani na ule wa Nyayo, kuwa ni baadhi tu ambazo zinapaswa kutoa huduma za mazoezi bila malipo.

Next read

Syokimau Homeowners Pool Funds For Water Solutions As Developer Pushes Back To Retain Control

19 September 2026 · 5 min read

Luxore Apartments in Syokimau, where homeowners are embroiled in a dispute with the developer over water supply.