Shirika la Kujenga Elimu ya Watoto wa Wafugaji

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Shirika la Kujenga Elimu ya Watoto wa Wafugaji

Kenya Drylands Education Fund (KDEF), shirika lisilo la kiserikali, linatumia teknolojia kusajili na kuhifadhi wanafunzi katika kaunti za Marsabit na Samburu.

Kituo cha Elimu ya Chekechea cha Nairabala, kilichoko umbali wa kilomita 13 Kaskazini mwa mji wa South Horr, ni mojawapo ya vituo 10 vilivyojengwa na KDEF kupiga jeki elimu ya watoto wa wafugaji katika kaunti za Marsabit na Samburu.

Umbali wa shule, unaoambatana na ukame, pamoja na mila na desturi za kitamaduni, vimesalia kuwa vikwazo vikubwa kwa upatikanaji wa elimu katika maeneo mengi ya kaunti za Marsabit na Samburu.

“Serikali ina uwezo wa kupata sajili ya shule ya kila siku, lakini kuna mapungufu katika mawasiliano miongoni mwa washikadau. Hili ndilo pengo tunaloziba kupitia rejista ya shule ya kidijitali,” alisema Ahmed Kura, mkurugenzi wa KDEF.

“Programu hii ya kidijitali husaidia shule za msingi kufuatilia mahudhurio kwa utaratibu. Inafanya kazi pamoja na programu ya kukusanya data nje ya mtandao iliyoko kwenye kompyuta kibao. Mfumo huo unaweza kumfahamisha chifu wa eneo hilo na washikadau wengine husika ikiwa mwanafunzi ameacha shule au hayupo kwa zaidi ya siku 10,” alisema Kura.

“Chifu anapopewa taarifa anafaa kuwatafuta watoto hao na kuhakikisha wanarejea shuleni. Tumeona kuwa idadi ya watoto wanaosalia shuleni imeongezeka kutokana na hatua hiyo,” alisema Kura.

Next read

LendPlus Employees Expose Staff Intimidation, Toilet Break Restrictions, Forced Overtime, Denial of Sick Leave and Threats of Dismissal at Digital Credit Provider

23 November 2026 · 3 min read

LendPlus employees expose toilet break bans, verbal abuse, forced overtime, denial of sick leave and threats of dismissal at the...